Showing posts with label miaka 50 ya uhuru. Show all posts
Showing posts with label miaka 50 ya uhuru. Show all posts

EDUCATION AND LITERACY 50 YEARS AFTER INDEPENDENCE: REFLECTIONS FOR ACTION 28-30th NOVEMBER 2011 SAVE THE DATE




!










Taasisi ya Usomaji na Maendeleo--
Soma
S.L.P 4460,
Dar es Salaam
Simu: +255754275347
Barua pepe: demeredye@gmail.com
!
Chama cha Wauza Vitabu
Tanzania (BSAT)
S.L.P 80174,
Dar es Salaam
Simu: +255754283866
!
21 NOVEMBA 2011
TAARIFA KWA UMMA
MAJADILIANO YA WAZI JUU YA ELIMU NA KUFUTA UJINGA
Mazungumzo ya kisera miaka 50 ya Uhuru: Hatua na mstakabali wa
elimu na kufuta ujinga nchini Tanzania.
Taasisi ya Usomaji na Maendeleo ya E&D —Soma na Chama cha Wauza Vitabu wa Tanzania
(BSAT) zinajihusisha na harakati za kufuta ujinga kwa njia ya kuhimiza usomaji na maendeleo ya
vitabu. Dira ikiwa ni kuiona Tanzania ikitimiza malengo yake ya maendeleo kama ilivyojiwekea
katika malengo ya milenia na MKUKUTA. Tunaamini jambo hili linaweza kufanikiwa kama
tutatafakari kwa umakini mstakabali wa elimu yetu: falsafa, ruwaza, na utendaji kwa kuzingatia
ubora, ushiriki, rasilimali, uendeshaji na vipaumbele inavyowekewa.
Katika kutimiza hilo, taasisi hizi zimeandaa, kama muendelezo wa Tamasha la VIitabu, mjadala wa
wazi utakaofunguliwa jumatatu ya tarehe 28 Novemba 2011 na kufungwa jumatano tarehe 30
Novemba 2011 muda ukiwa ni saa 11:00 jioni hadi saa 4:00 usiku kwa siku zote ili kutafakari hatua
zilizopigwa na wadau mbalimbali katika elimu na kufuta ujinga ndani ya miaka hamsini baada ya
uhuru wa Tanganyika. Majadiliano haya yatafanyika katika viunga vya Mkahawa wa Vitabu Soma
(Mtaa wa Regent Estate, Kitalu Na. 53, Mlingotini Close) kama sehemu ya Tamasha la Vitabu.
Madhumuni ya majadiliano haya ni kutoa fursa kwa wadau mbalimbali wa elimu: wanajamii,
waelimishaji, watekelezaji na watunga sera, wanataaluma, wanazuoni, pamoja na wanafunzi,
kutafakari kwa kina kuhusu juhudi za wananchi na Serikali tangu enzi za Mwalimu Nyerere katika
kufuta ujinga kama mojawapo ya maadui watatu wa maendeleo yetu.
Mdahalo utafanyika jumanne tarehe 29 Novemba 2011 huku ukihusisha tafakuri ya kina
itakayofungamana na vionjo vya kisanaa, ukiwaleta pamoja wadau wenye stadi, mitazamo, na
uzoefu mbalimbali katika elimu kuzungumzia hatua tuliyopiga katika maendeleo ya elimu na
juhudi za kufuta ujinga. Maswali makuu yatakuwa: “kipi tumefanya vyema?”, “kipi tungeweza
kufanya vyema zaidi?” na “nini tunahitaji kufanya?” ili ndani ya muongo mmoja tuweze kuwa
mfano bora wa jamii inayojua kujifunza.
Mbali na hivyo, kuanzia jumatatu yatakuwa yakifanyika matukio kwa ajili ya jamii nzima kama vile
maonesho ya vitabu na huduma za kielimu, vionjo vya kifasihi kama vile mashairi, ngonjera,
ngano; shughuli za kuchangisha fedha kwa ajili ya huduma za kielimu ikiwemo ujenzi wa maktaba
za jamii na mashindano ya fasihi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari, mnada wa vitabu
vilivyotumika, maonesho ya muziki, dansi, nyama choma, na vinywaji.
Hivyo basi, tunatoa rai kwa jamii nzima na watu wote wahudhurie kwa wingi bila kukosa kwa siku
zote tatu ili kuja kubadilishana mawazo na watu wengine wenye maono na mitazamo tofauti
kuelekea kuboresha hali ya elimu nchini. Hapatakuwa na kiingilio chochote kwa siku zote tatu.
! ! ! ! ! !
Demere Kitunga-(SOMA)
!
Hobokela Magale-(BSAT)
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Miaka 50 ya Uhuru -hata wajawazito sasa tutapeleka India kujifungua?????


Tunaadhimisha miaka 50 tangu Tanganyika ipateuhuru wake kwa mkoloni, lakini licha ya kujivunia kwa mambo lukuki kuwa TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA SASA NCHI INASONGA MBELE lakini katika hili la afya hasa wodi za akina mama waja wazito bado hatujaweza kuondopa kero ya vitanda na wodi katika Hospitali zetu nyingi. Serikali haina budi kuamka sasa na kunadi shangingi 1 kila Wizara au Taasisi kubwa ili kununua hata vitanda na kujenga Wodi za akina mama hawa. Isipofanyika hili haraka itafikia hatua kiongozi fulani akitaka kujifungua atapelekwa India maana huduma zetu hazikidhi kiwango
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Maonyesho ya Wizara ya Fedha ya miaka 50 ya uhuru



Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Mali za Serikali(CHC) Dome Malosha
akipokea kikombe cha ushindi wa jumla wa kwanza wa maonyesho ya Wizara
ya Fedha ya miaka 50 ya uhuru kutoka kwa Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo jana jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha Mustafa Mkulo akizindua kitabu cha historia ya Wizara ya
Fedha jana mjini Dar es salaam kwenye maonyesho ya Wizara ya Fedha ya
miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara yanayoendelea katika viwanja vya
Mnazi mmoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa
Dkt. Albina Chuwa akitoa ufafanuzi kwa mwananchi jana jijini Dar es
salaam wakati mwananchi huyo alipotembelea banda la Ofisi ya Taifa ya
Takwimu katika maonyesho ya Wizara ya Fedha ya miaka 50 uhuru wa
Tanzania bara.
Waziri
wa Fedha Mustafa Mkulo akisoma hotuba ya ufunguzi rasmi jana mjini Dar
es salaam maonyesho ya Wizara ya Fedha ya miaka 50 ya uhuru wa
Tanzania bara yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi mmoja.
Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

SHULE YAKOSA CHOO MAGONJWA YA MLIPUKO YATISHIA, NA WATOTO WAKETI SAKAFUNI WAKIHITAJI ELIMU BORA.


Hiki ndicho choo wanachotumia wanafunzi wa shule ya msingi Mpakani iliyopo mjini Tunduma majaaliwa yao yakoje? wanasoma wakiwa wameketi sakafuni, Tunduma ni moja ya miji maarufu nchini kwa biashara kati ya Tanzania na nchi zilizopo kusini mwa Afrika, ni mji wenye msongamano mkubwa wa biashara.


Jamani haiwezekani kwa hili pia magonjwa ya Mlipuko kutishia eneo hili, Wizara husika tazameni kwa macho ya huruma na kutekeleza pia ahadi Mashuleni.


Huenda watoto hawa ni wa wafanyabiashara wanasoma kwa kuketi chini,wanaweza kuwa wazazi wao ndio wamiliki wa maduka yanayozunguka katika mji maarufu wa Tunduma, wametelekezwa?serikali iko wapi mbona imewatelekeza watoto hawa?

Chanzo: Mbeya yetu
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

SHEREHE ZA KUWASHA MWENGE WA UHURU NA KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA KIJIJINI BUTIAMA LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa uhuru kiongozi wa mbia za mwenge huo mwaka 2011 2012 Mtumwa Rashid Halfan kutoka mkoa wa kaskazini Unguja, kwa ajili ya kuanza mbio za kukimbiza katika mikoa yote ua Tanzania baada ya kuuwasha rasmi leo katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la mauwa kwenye Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere baada ya misa maalum ya kumkumbuka muasisi huyo Taifa la Tanzania iliyofanyika leo kijijini kwake Mwitongo Butiama.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzinduwa kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza iliyoambatana na maadhimisho ya miaka 50 Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mara. Kulia Waziri wa Habari utamaduni na Michezo Mhe. Dkt Emanuel Nchimbi na kushoto ni Naibu waziri katika wizara hiyo Dkt Fenella Mukangara


Mwandishi wa Habari na mpiga picha mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Bi. Anna Itenda, kwa niaba ya waandishi wa habari wa Tanzania, akiweka shada la mauwa katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere wakati wa misa maalum ya kumkumbuka muasisi wa Taifa la Tanzania iliyofanyika jana kijijini Mwintongo Butiama.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

KILELE CHA UWT NA MIAKA 50 YA UHURU NA KUMBUKBMU YA MWL NYERERE-MUSOMA

Baadhi ya mabango yenye ujumbe yakionyeshwa katika kilele Tarime


Hawa ni baaddi ya waasisi wa UWT


Karibu tena Mama yetu Mkoani Musoma- Mbunge viti maalumu Mkoa wa Mara Rosemary Kirigini baada ya kualizika sherehe Tarime


katibu Mkuu wa UWT Amina Makillagi (shoto) akimtambulisha muasisi Dr, Msimu Abdulrahman Hassan.


Kikundi cha kwaya ya Chuo cha ualimu Tarime


Mama Karume (shoto) na Mama Salma Kikwete wakiwaaga UWT babada ya kumalizika sherehe Tarime za UWT Kitaifa



Muasisi wa UWT Zanzibar Mama Fatma Karume akionyesha Tuzo yake baada kutunikiwa


Muasisi wa UWT Zanzibar Mama Fatma Karume (kulia) na Mama Kikwete wakifurahia maonyesho ya wajasiriamali Tarime.
Picha zote na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»