Showing posts with label nape. Show all posts
Showing posts with label nape. Show all posts

NAPE AKISALIMIANA NA WAZEE WA CCM


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimsalimia Mbunge wa Monduli na Mjumbe wa NEC, Bw. Edward Lowassa. wakati wa kikao cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Ukumbi wa White House mjini Dodoma jana. Kulia kwa Bw. Lowassa ni Waziri Mkuu Mstaafu Bw. Fredrick Sumaye na Bw. Kingunge Ngombale Mwiru (kulia)
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Nape Nnauye atinga Ukerewe


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Getrude Mongela mjini Nansio, Ukerewe mkoani Mwanza
Sehmu ya Umati Mkubwa wa Wanaccm Ukerewe Wakimsiliza Nape Nnauye
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe, Queen Mlozi (kulia) akimpa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape alipofika kwenye Ofisi ya CCM ya wilaya hiyo, jana. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Queen Mlozi baada ya kuwasili jana kwenye Kivuko cha Nansio Ukwewe kwa ajili ya ziara ya siku moja wikayani humo.
Nape akivishwa skafu na Chipukizi wa CCM baada ya msafara wake kuwasili Kivuko cha Nanisio, jana.
Nape akipinga ngoma kuunga mkono kikundi kilichokuwa kikitumbuiza kwenye mkutano huo.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

NAPE AUNGURUMA KATORO, GEITA


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika stendi ya mabasi Katoro, Geita.
Nape, Mwigulu na Mbunge wa Mtera Livimgstone Lusinde wakitoka katika mkutano huo, uliofanyika Stendi ya Mabasi, Katoro, Geita.
Aliyekuwa Katibu wa Uenezi wa CHADEMA Kata ya Katoro Anastazia Marwa akimkabidhi kadi ya chama hicho Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye alipotangaza kuhamia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Stendi ya Mabasi, Katoro, Geita. Anastazia alikuwa pia Katibu wa Barza la CHADEMA jimbo la Busanda, Geita.
KIna mama wakimshangilia aliyekuwa Katibu wa Uenezi wa CHADEMA Kata ya Katoro Anastazia Marwa baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Stendi ya Mabasi, Katoro, Geita. Anastazia alikuwa pia Katibu wa Barza la CHADEMA jimbo la Busanda, Geita. Anastazia baada ya kutangaza kuhamia CCM katika mkutano huo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya John Mass, akionyesha umahiri wake, alipotumbuiza katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika leo kwenye Stendi ya Mabasi, Katoro, Geita.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Nape ‘avamia’ ngome ya Chadema

AZOMEWA, GREEN GUARD WATEMBEZA KIPIGO



Frederick Katulanda, Mwanza
Nape Nnauye
MKUTANO wa hadhara wa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Magoneni, Kirumba jijini hapa, uliingia dosari baada ya kundi la vijana kuwazomea viongozi karibu wote wa chama hicho waliopanda jukwaani na kukifanya kikundi cha ulinzi cha CCM, Green Guard kutembeza kipigo hadharani.Katika mkutano huo, Nape alikuwa amefuatana na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde, Katibu wa Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Nzega Dk Hamis Kigwangalla.

Baada ya kuanza saa 9: 55, Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Shaibu Akwilombe ambaye pia ni Katibu wa Wilaya ya Ilemela alipanda jukwaani kuwatambulisha makada wa chama hicho waliokuwa katika msafara wa Nape kisha kumkaribisha Dk Kigwangalla kuzungumza.

Akizungumza katika eneo hilo ambalo ni moja ya ngome maarufu za Chadema, Dk Kigwangalla alisema katika zama za sasa hakuna chama kinachoweza kuwafikisha wananchi katika uchumi mwema zaidi ya CCM. Kauli hiyo ilionekana kuwakera baadhi ya wananchi hasa vijana walikuwapo katika mkutano huo ambao walianza kuzomea huku wengine wakiguna.

Kuona hivyo, Dk Kigwangalla alikatisha hotuba yake akisema yeye siyo msemaji wa mkutano huo. Akwilombe alirejea jukwaani, safari hii akionekana kujawa na hasira na kusema hatakubali kuona watu wakileta vurugu na kusema wanaofanya hivyo wanapima kina cha maji kwa kuweka mguu.

“Hata bila ya polisi hatuwezi kukubali fujo zitokee katika mkutano wetu… na sasa namkaribisha Lusinde kuwasha moto na wanaotaka kupima kina cha maji kwa mguu waone..,” alisema Akwilombe.

Lusinde aliposimama alisema kelele za kuzomea amezizoea na amejifunzia Tarime ambako alikuwa Katibu wa CCM hivyo hazimpi shinda.

“Hawa wanajifunza kutoka Tarime, wanaiga mambo ya utoto, huu mkutano siyo wako ni mkutano wa CCM wewe unakuwasha nini? Kama unaona huwezi kuvumilia mwana CCM usiende kwenye mkutano wa Chadema na kama mwana Chadema huwezi kuvumilia mkutano wa CCM usiende! Wanachofanya ni kwamba uvumilivu kwa vijana wa CCM unafika mwisho,” alisema.

Kauli hiyo ilikuwa kama kutia petroli kwenye nyasi zinazowaka kwani ilizidisha vurugu huku zomeazomea ikiongezeka baada ya hali hiyo kuendelea, Lusinde alisema: “Hii ni nchi yetu wote kilichotokea hapa (Kata ya Kirumba kuongozwa na upinzani), wanakijua, lakini lazima wajue hakuna watu wenye haki ya kuzunguka nchi nzima na wengine wakakosa.”

Ilipofika zamu ya Nchemba ambaye alikuwa Mratibu wa uchaguzi mdogo wa CCM, Igunga alisema Chadema kimeshindwa Igunga kihalali na kwamba anashangaa kusikia kikilalamika kuibiwa kura.

Alisema katika uchaguzi huo hakuna masanduku ya kura yaliyopotea wala kituo ambacho kura zake hazikuhesabiwa. Alidai kwamba kama Chadema kisingefanya hujuma, kisingepata kura zaidi ya 1,000.

Baada ya Nchemba iliwadia zamu ya Nape. Vurugu zilitokea mara mbili wakati kiongozi huyo machachari wa CCM alipokuwa akihutubia.

Nape alianza kwa kuwapongeza Nchemba na Lusinde akisema walipokuwa wakizungumza walikuwa wakikamata pua za wagonjwa wakorofi ili yeye aweze kuwanywesha dawa.

Wakati akihutubia, vijana wa Green Guard walianza kufanya doria kuwasaka wazomeaji na kijana wa kwanza alikamatwa na kushambuliwa na vijana zaidi ya saba kiasi cha kumfanya Nape kukatisha hotuba yake kumuokoa.

Hali ilichafuka tena pale aliposema viongozi wa upinzani hawana uchungu na nchi na kwamba CCM ni waungwana na ndiyo maana Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Katibu wake Mkuu, Dk Wilibroad Slaa hawajawahi kuguswa kwa risasi huku akiwahoji kuwa tangu siasa za vyama vingi zianze ni wapi ambako viongozi hao walifanyiwa hivyo? Hata hivyo, alijibiwa kwa nguvu na kundi la watu ... “Arusha.”

Majibu hayo yalisababisha vurugu nyingine kwani kijana mwingine alikamatwa na kuanza kupigwa na vijana hao wa CCM kabla ya gari la Polisi kuwasili na kuanza kuzunguka katika uwanja huo kulinda amani.

Mkutano huo unadaiwa kuwa ni wa maandalizi ya kampeni za kuwania kiti cha udiwani wa Kata ya Kirumba ambacho kipo wazi baada ya diwani wake, Novatus Manoko (Chadema) kufariki dunia.

CHANZO: MWANANCHI
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Nape Nnauye Azuru Kaburi La Baba Yake, Ateta na Rais Jakaya Kikwete


Rais Jakaya Kikwete akiagana na viongozi wa ngazi za juu wa CCM baada ya mazishi ya Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Uhuru FM Juma Penza, jana katika makaburi ya Kisutu mjini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimwagilia maji kwenye kaburi la Baba yake Marehemu Mussa (Mosses) Salum Nnauye kwenye makaburi ya Kisutu mjini Dar es Salaam, jana.


Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa kwenye kaburi la Baba yake Marehemu Mussa (Mosses) Salum Nnauye kwenye makaburi ya Kisutu mjini Dar es Salaam, jana.Picha Zote na Mdau Picha zote na Bashir Nkoromo-Uenezi CCM
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

KUMBUKUMBU YA MIAKA 12 YA KIFO CHA MWALIMU NYERERE


KAMANDA wa Vijana Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, Sharik Choughule, akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam.


KATIBU wa Siasa na Uenezi tawi la CCM, Mchafukoge, akimkumbuka Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya miaka 12 ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam.
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Mpasuko CCM sasa dhahiri

MWENYEKITI ARUSHA AMSHAMBULIA NAPE,AMWITA MUASI WA KWANZA, WARIOBA AONYA




Waandishi Wetu
HALI imezidi kuwa tete ndani ya CCM na sasa mpasuko ambao umekuwa ukitajwa kukigawa chama hicho kikongwe nchini ni dhahiri. Hali hiyo inatokana na hatua ya makada na viongozi wake waandamizi kurushiana maneno makali nje vikao vyake rasmi kama ambavyo awali kilikuwa kimejenga msingi imara wa taratibu za kumaliza mambo yake ya ndani kimyakimya.

Jana, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole aliibuka na kumshambulia hadharani Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye akimwita: “Muasi namba moja.” Nangole alikuwa akijibu kauli ya Nape aliyoitoa wiki hii akisema ndani ya chama hicho kuna kundi la waasi wanaokihujumu chama na hasa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Akijibu shutuma hizo jana, Nape alisema: “Ukirusha jiwe kwenye giza, halafu ukasikia mtu akiguna ujue huyo ndiye uliyemponda. Sasa mimi kwenye press release (taarifa kwa vyombo vya habari) sikutaja jina la mtu wala mkoa, sasa iweje yeye leo aanze kujibu?”

“Ninamheshimu sana Mzee Nangole lakini sidhani kama waliomshauri kutoka wamemshauri sawasawa, kama anaweza namshauri akasome taarifa yangu halafu aje tena kwenye press (vyombo vya habari), atazungumza vizuri,” alisema Nape.

Malumbano hayo baina ya Nangole na Nape wote wakiwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), yamekuja siku moja tu tangu mwanasiasa mkongwe nchini, Jaji Joseph Warioba alipovionya vyama vya siasa nchini hususan chama hicho tawala kutokana na kile alichokiita kuwa ni “kukosekana kwa nidhamu ya kuzungumza.”

Katika mahojiano na Kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC1), Warioba alisema hali katika vyama vya siasa inasikitisha kwani kumekuwa na malumbano makali baina ya viongozi.

Jaji Warioba aliyepata kuwa Waziri Mkuu alisema hali hiyo inakiathiri zaidi CCM ambacho ni chama tawala na akahoji sababu za kuachwa kwa misingi ya mwanzo ya kuzungumza kwa nidhamu mambo yanayokihusu chama hicho.

“CCM kinaathirika zaidi na hali hii ya kutokuwepo kwa nidhamu ya kuzungumza ndani ya vyama, maana chenyewe kiko madarakani, unashangaa kimetokea nini kwa chama ambacho kilikuwa na nidhamu ya hali ya juu ya kuzungumza,” alisema Warioba.

Kauli ya Nangole
Nangole katika mkutano wake na waandishi wa habari jana alimtaka Nape aachane na malumbano yasiyo na tija ndani ya chama na badala yake asisitize utekelezaji wa Ilani ya CCM kwani malumbano hayo yanaashiria dalili mbaya za anguko la chama hicho siku zijazo.

Alimtaka Nape ajikite kutangaza mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na chama hicho badala ya kuendeleza malumbano kila kukicha.
“Tufanye shughuli za kukijenga chama. Mimi nilidhani Nape atakuwa akisisitiza utekelezaji wa Ilani za chama lakini yeye kila siku ni 'gamba, gamba tu.' Haya yatatufikisha wapi? Watu wanataka maendeleo,” alisema Ole Nangole. Alisema ndani ya CCM kwa sasa kumekuwa na makundi mbalimbali ambayo yanasigana bila tija huku akionya kuwa dalili hizo za makundi zitaifikisha pabaya.

Akizungumzia kauli ya Nape kwamba kuna uasi ndani ya CCM, Mwenyekiti huyo wa Mkoa alisema ikiwa ni kweli, basi uasi wa kwanza ulifanywa na Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM, kwani aliwahi kutajwa kuwa mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ).

Alisema mara kwa mara Nape amekuwa akituhumiwa na baadhi ya makada wa chama hicho akiwamo aliyewahi kuwa Mbunge wa Kishapu, Shinyanga, Fred Mpendazoe kuwa ni miongoni waanzilishi wa CCJ na hivyo kutamka kuwa kama ni suala la uasi basi Nape huenda akawa wa kwanza kuasi CCM.

Ziara ya UVCCM
Mwenyekiti huyo alipongeza ziara iliyofanywa na wanachama wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) hivi karibuni mkoani Arusha, ambayo kimsingi ndilo chimbuko la malumbano yanayoendelea hivi sasa.

Alisema ziara hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Benno Malisa ilipaswa kupongezwa kwa kufufua uhai wa chama wilayani Arusha badala ya kubezwa hasa ikizingatiwa kuwa wakati huu, chama cha upinzani, Chadema kimeweka himaya yake maeneo mengi ya Mkoa wa Arusha.

Hata hivyo, alisema chanzo cha migogoro hiyo ni chuki mbalimbali ndani ya CCM zinazosababishwa na vita ya urais mwaka 2015 na kwamba huenda ikakimaliza chama hicho kwa kukiweka pabaya kwenye uchaguzi huo.

“Chuki zote za kuchafuana ni maandalizi ya 2015 na hili ndilo linachangia kutumaliza. Hebu tutekeleze Ilani ya chama. Nawapa pole wanaosaka urais kwa sasa kwani bado mbali sana,” alisema.
Kauli ya Nape Kwa upande wake, Nape alikanusha kuzungumzia ziara ya UVCCM Arusha katika mkutano wake na waandishi wa habari: “Naomba nieleweke, sijawahi kuzungumzia ziara ya umoja wa vijana mkoani Arusha, kwa hiyo madai yoyote yanayohusiana na suala hilo si yangu kwa sababu wanataka kunihusisha na jambo ambalo sihusiki nalo.”

“Kama nilivyosema sikutaja jina la mtu wala mkoa, sasa kwa nini leo hii wasijibu wenyeviti wa Mwanza, Shinyanga, Morogoro au kwingineko na ajibu yeye?”

Kuhusu mbio za urais wa 2015, Nape alisema: “Sijui kwa nini haya mageuzi ya kujivua gamba yanapotajwa yanahusishwa na urais. Hili si sahihi hata kidogo. Kwa mfano, unanihusisha mimi Nape na wagombea watano, hata kama ningekuwa nashabikia hili, nitakuwa vipi na wagombea wote hawa?,”

Alisema Sekretarieti ya CCM inayoongozwa na Katibu Mkuu, Wilson Mukama imekuwa na kazi nyingi za chama na si kutafuta mgombea wa urais wa 2015 na kwamba hao pengine wanaolizungumza kila wakati ndiyo wenye wagombea wao.

Alipoulizwa CCM kutokuwa na utaratibu wa kutoa taarifa Nape alijibu: “Sasa ninyi mngekuwa mkinisaidia kuwahoji hao, kwamba wanazungumza kama kina nani, maana utaratibu wa chama unaeleweka na msemaji wa chama anafahamika.”

Kauli nyingine
Oktoba 12 mwaka huu, Nape aliwaambia waandishi wa habari kuwa kumeibuka kundi la watu wenye nguvu ya fedha wanaokisaliti chama kwa kuendesha propaganda za kupotosha dhana ya kujivua gamba.

Alisema kundi hilo linamhujumu pia Rais Kikwete lakini akasema chama kimejipanga kuwashughulikia wanaounda kundi hilo.

Alipotakiwa kutaja hujuma za kundi hilo dhidi ya Mwenyekiti wa CCM, Nape alisema: “Ni nyingi, moja ni kusambaza hoja ya kutaka nafasi ya urais itenganishwe na ile ya mwenyekiti wa chama.”

Nape ilitoa matamshi hayo siku chache tangu Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM, Beno Malisa atoe kauli ya kukikosoa chama na Serikali yake akiwataka makada wa CCM kuacha kuingilia siasa za Chadema na pia kuitaka itafute suluhu ya matatizo yanayokabili wananchi.

Benno alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara Mjini Arusha, eneo ambalo linaonekana kuwa chimbuko la malumbano yanayoendelea hivi sasa ndani ya CCM.

Mkutano huo ndiyo pia chimbuko la tukio la Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha, James Ole Millya kusakwa na polisi kwa tuhuma kwamba alitoa matamshi yenye kuchochea vurugu.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa alisema jeshi hilo linamsaka Ole Millya kuhusu kauli yake kwamba mtoto mmoja wa kigogo alitoa maagizo kwa polisi kuzuia UVCCM wasifanye mkutano siku hiyo.


Msuguano wa ndani
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na misuguano ndani ya chama hicho, huku kukiwa na kundi ambalo linadaiwa kuwa na ajenda dhidi ya utekelezaji wa falsafa kujivua gamba iliyopitishwa na NEC ya CCM ikiwataka watuhumiwa wa ufisadi kuachia nyadhifa zao.

Habari kutoka ndani ya CCM zinasema kundi hilo la waasi linaungwa mkono na wenyeviti wa CCM wa mikoa zaidi ya 10 na kwamba ndilo linalosukuma ajenda ya kutaka kutenganishwa kwa kofia ya Rais na Mwenyekiti wa CCM.

Habari zaidi zinasema kuwa baada ya uchaguzi wa Igunga, kundi hilo lilipata nguvu zaidi kutokana na kuanza kuungwa mkono na mmoja wa makada wa siku nyingi wa chama hicho kutoka moja ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Miongoni mwa mikakati ya kundi hilo ni kuhakikisha ajenda ya kuteganishwa wa nafasi hizo mbili inafanikiwa, kufutwa kwa mpango wa kujivua gamba na kumng’oa Nape katika nafasi yake ya sasa kwa madai kwamba anakiharibu chama.

Habari hii imeandikwa na Moses Mashalla, Arusha na waandishi wetu Dar
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

CCM wakiri hawakustahili ushindi


NAPE ASEMA WAMEPENYA TUNDU LA SINDANO



Na Efracia masaweCHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekiri kuwa hakikustahili kushinda katika uchaguzi mdogo uliomalizika jimboni Igunga mwanzoni mwa mwezi huu.

Badala yake, kilisema waliopaswa kushinda ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho kilikuwa kinaungwa mkono na wananchi wengi.
Hata hivyo, CCM imedai kwamba ushindi wake Igunga umetokana na CHADEMA kutumia vitisho, ikiwamo kumkamata na kumwadhibu Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, aliyekutwa anakula njama za ushindi wa CCM.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, katika mkutano wa mapokezi ya mbunge aliyechaguliwa, Dk. Peter Kafumu, katika viwanja vya Bakhresa, Manzese, Dar es Salaam.
Dk. Kafumu alishinda kwa tiketi ya CCM kwa kura 26,484 dhidi ya 23,260 za mgombea wa CHADEMA, Joseph Kashindye. Vyama vingine sita, kikiwamo CUF, vilipata kura chache sana ambazo katika jumla yake hazifiki hata 2,800.
Nape alisema: “Kama CHADEMA wasingejihusisha na vitendo vya kikatili, basi leo hii chama hicho kingekuwa madarakani. Nakiri wazi kuwa CHADEMA wangeweza kuchukua kura zaidi ya 5,000 Igunga…
“Tumeshinda kupitia tundu la sindano, hiyo ipo wazi kabisa… CHADEMA waliwateka wananchi kwa asilimia zote. Kosa lao la kwanza waliwakashifu siku moja kabla ya kupiga kura kwa kuwaleta wasomi ili waje wahesabu kura kwa usahihi, hapo ndipo tatizo lilianza.”
Alisema CHADEMA ilikuwa imewateka wananchi wa Igunga, lakini baadaye walikerwa na kitendo cha chama hicho kuingiza walinzi wa kura kutoka nje ya jimbo.
“Nawahakikishieni baadhi ya wanachama waliokerwa na kitendo hicho cha kutokuaminiwa, kiliwafanya kundi kubwa la wanachama hewa wakichague chama cha CCM, tukaongezewa kura, ” alisema Nauye.
Naye Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Kafumu alitumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wote waliomchagua na akaahidi kuwa nao bega kwa bega katika ufanisi wa kazi.
“Nitawatumikia bila ubaguzi wa chama au mtu yeyote. Nawashukuru kwa kila jambo na Mungu awabariki katika shughuli zenu; naomba tuendelee kushikamana,” alisema Kafumu
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»