DKT DAVID MARSHALL MOSHA AFARIKI DUNIA LEO HUKO KABUKU, KOROGWE



Dkt. David Marshall Mosha (pichani), Mwenyekiti Mstaafu wa Bodi za Wakurugenzi wa kampuni ya Ujenzi ya Inter-Consult pamoja Akiba Commercial Bank, amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo kiasi cha saa Tano asubuhi katika mji wa Kibuku, kilometa kadhaa toka Korogwe, mkoani Tanga.


Mmoja wa Wakurugenzi wa Inter-Consult Dkt. Startto P. Mosha kathibitisha habari hizo punde, na kusema kuwa mareheu alikuwa akisafiri yeye na dereva wake kutoka Dar es salaam kuelekea Moshi, kabla gari lake aina ya Toyota Double Cabin halijaacha njia na kupinduka kwa sababu ambazo bado hazijajulikana.


Dkt Stratto Mosha amesema mipango ya mazishi itafanywa baada ya mwili wa marehemu ambao uko katika chumba cha maiti cha hospitali ya Wilaya ya Korogwe utapoletwa nyumbani kwake Mbezi Chini, karibu na mafleti ya BOT, na kwamba tayari timu imeshaondoka kwenda Korogwe.


Amesema dereva wa marehemu yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi na hali yake inaelezwa kuwa ina 'stabilise' .


Kwa mujibu wa Dkt. Stratto Mosha, marehemu alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi kwa miaka 12 kabla ya kustaafu mwaka 1978 na kubakia Mkurugenzi. Pia ameitumikia Akiba Comercial Bank kwa miaka 10.kabla ya kustaafu mwaka jana na kubakia mjumbe wa bodi hiyo.

Categories: