Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano-Mallya akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari za michezo kutoka makampuni tofauti ya habari kuhusu Kliniki ya Airtel Rising Stars itakayo fanyika katika uwanja wa taifa hapa Dar es salaam chini ya usimamizi wa Makocha wa Manchester United. Kliniki hiyo itajumuisha vijana kutoka Kenya, Malawi, Seirra Leone na Tanzania. Kliniki hiyo itaanza tarehe 30 Oktoba na kuisha tarehe 3 Novemba. Kilia ni Afisa Mahusiano wa Airtel Jane Matinde (kushoto) AON Financial Controller Deepna Shah.
|