Gari la mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa likiwa limeingia nyuma ya gari ambalo lilikuwa mbele yake kabla ya dereva wa gari hilo la mbele kuamua kurudi nyuma ghafla na kuligonga gari hilo la mbunge
Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (chadema) leo amenusurika katika ajali ya gari baada ya gari lake kugongana na gari jingine ambalo lilikuwa mbele yake kabla ya wa dereva wa gari hilo ambalo lilikuwa likiingia barabara kuu kuamua kurudisha nyuma ghafla gari lake na kuligonga gari hilo na mbunge.
Tukio hilo limetokea leo majira ya mchana wakati mbunge Msigwa akitoka katika kuwatumikia wananchi wake wa jimbo hilo.
Hata hivyo katika ajali hiyo gari la mbunge Msigwa halikuharibika sana ukilinganisha na gari hilo lililo rudi nyuma na kumgonga.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN BLOG
Categories:
mbunge,
Mbunge Peter Mwesigwa