Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai Mh Freeman Mbowe akisikiliza maelezo ya mhandisi , Pissy juu ya namna ya kumaliza tatizo la ubovu wa barabara inayoelekea kwenye kituo cha Afya cha Kisiki ambapo Dr mkuu wa kituo hicho ,Isdory Kavishe (mwenye koti jeupe) naye alimshukuru mbunge huyo kwa kuamua kushughulikia tatizo hilo kwa kile alichosema kuwa imekuwa ikipitika kwa shida hasa kipindi cha mvua kutokana na utelezi
Mh. Mbowe akikagua kivuko cha miguu cha Miase nikinachounganisha kitongoji cha Mwara na Mashare ambacho kinahitaji kufanyiwa matengenezo baada ya kingo zake kumomonyoka kutokana na mvua zilizonyesha hizi karibu huku kukiwa na hitaji ya kukibadilisha kukitengeneza kwa kutumia reli.
Mbowe akisikiliza malezo ya mwenyekiti wa kijiji cha Nshara , Awadhi Uronu (aliyekunja mikono) kuaharibika kwa kivuko cha waenda kwa miguu kilichoharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni , aliambatana na mwenyekiti wa halmashauri hiyo , Clemence Kwayu (mwenye Kaunda suti nyeusi). Picha na Habari na Grace Macha
******
MWENYEKITI wa Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe yuko kwenye ziara ya wiki mbili jimboni kwake kukagua miundo mbinu ya barabara za vitongoji na vijiji akiwa ameambatana na mhandisi wa halamshauri ya Hai Bw. Cosmas Pissy na wataalamu wengine wa idara hiyo .
Kazi kubwa ilikuwa ni kutathmni maeneo korofi kwa lengo la kuyawekea mkakati maalum wa kuyatengeneza kwa kuainisha aina ya marekebisho yanayohitajika na gharama zake ili ziweze kutengenezwa .
Alipita kukagua barabara inayopita pembeni ya soko la Kalali ambapo wanachi waliacha shughuli zao na kumfuata huku wakimweleza kuwa wanaendelea kutozwa ushuru wa soko wakati ulishafutwa ambapo Mbowe aliahidi kulishughulikia suala hilo kwa kuongea na Mkurugenzi wa halmashauri ili amweleze ni kwa nini wanaendelea kutoza ushuru wakati tayari walishaufuta kupitia kikao cha baraza la madiwani na walikubaliana kuanzia Oktoba mwaka huu usitozwe kwa wale wenye kuuza bidhaa ndogondogo kwenye masoko yote ya wilaya hiyo.
Categories:
chadema,
mh Freeman Mbowe