KOCHA WA YANGA KOSTADIN PAPIC ATUA JANGWANI KUKINOA KIKOSI HICHO KUCHUKUA NAFASI YA SAM TIMBE


Na Francis Dande

Katika kuhakikisha inashinda katika pambano lake dhidi ya mtani wa jadi Simba, Klabu ya Yanga imemrejesha kocha wake aliyekuwa akikinona kikosi hicho katika msimu uliopika wa Ligi 2010-11 kabla ya kukatisha mkataba wake, Pichani Kocha wa Yanga Kostadin Papic akitoka katika mazoezi ya timu hiyo baada kuifundisha timu hiyo kwa kipindi cha saa moja baada ya kuanza rasmi kazi hiyo akichukua mikoba ya aliyekuwa mtangulizi wake Sam Timbe ambaye mechi yake ya mwisho ilikuwa ya jana kati ya Yanga na JKT Oljoro ambapo yanga iliibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0.

Kocha huyo kutoka Uganda mkataba wake ulikuwa uishe mwezi mei 2012 ambapo alikuwa na jukumu la kuinoa timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, Kocha Papic mtihani wake wa kwanza utakuwa dhidi ya Simba katika mpambanmo utakaofanyika kwenye Uwanja wa taifa Oktoba 29.

Habari za uhakika kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa Sam Timbe tayari ameshapewa barua yake ili kumpisha Kondic. Hata hivyo kabla ya ujio wa Timbe,Papic ndiye aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.

Categories: , ,