WAFANYAKAZI WA TICTS WAGOMA,WAKISHINIKIZA KULIPWA MAFAO YAO


Wafanyakazi wa TICTS tokea jana wamekuwa na mgomo wa kufanya kazi katika Kitengo hicho Bandari wakishinikiza kulipwa madai yao ya Hisa ya zaidi ya miaka Miwili.



Mgomo ukiendelea



Sehemu ya Mabango yanayotumiwa na wafanyakazi hao wakati wa mgomo huo.

*****

Taarifa kutoka kwa wafanyakazi hao zinasema kuwa, licha ya kugoma kwao lakini uongozi wa Kitengo hicho bado haujawaita ili kupata suluhu ya tatizo hilo na badala yake umekutana na Uongozi wa wafanyakazi (Dowuta) TICTS pekee.

Wafanyakazi hao wanaodai kuwa wataendelea na Mgomo huo mpaka hapo watakapolipwa Stahili zao na Kitengo hicho.

Kufuatia mgomo huo shughuli zote za Kitengo hicho cha TICTS zimesimama Pia katika mgomo wao Hawataki baadhi ya viongozi wao kwa sababu ya unyanyasaji, wameomba serikali iingilie kati na ikiwezekana wawaondoe viongozi hao ambao Ni Biset Nevil, Anton,Mzungu wa Security,mama Prediganda Asenga na Abel Mwangwa maana hao ndo wachochezi wakubwa ili hisa zao wasipewe wagawane na mafisadi wa nchi hii na pia wanaomba serikali iingilie kati maana wazungu wao wanalipwa mishahara mikubwa na wakati kazi hufanya wao,utakuta mzungu mmoja analipwa dola za marekani elfu ishirini na sita $26,000 kwa mwezi huku wafanayakazi wakitaabika na kufukuzwa ovyo kama kuku.

"Bado mgomo uko pale pale mpaka kieleweke maana walikuwa wanasingizia serikali na wenye share ambao ni akina Karamagi na wengine sasa kama hao ndo chanzo basi waende wakaongee nao na watae sababu ya kuzuia hizo asilimia tano tulizosign nao mkataba kwamba wakifika miaka kumi watatupatia wafanyakazi asilimia tano"alisema mmoja wa wafanyakazi hao. Hizo ailimia tano zinathamani ya sh. billion 16.7

Categories: ,