WAZIRI NCHIMBI AWATAKA WATANZANIA KUZINGATIA MAADILI YA MILA NA DESTURI ZAO.






WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Emanuel Nchimbi ametaka Watanzania  kuzingatia maadili yatokanayo na Mila na desturi ikiwa ni pamoja na kudumisha mila zao. Waziri huyo alisema kuwa ikiwa Watanzania wataweza kudumisha mila na desturi zao hali hiyo itasaidia kuongezeka kwa maadili hususani kwa vijana ambao kwa hivi sasa maadili yamepungua kwa kiasi kikubwa.


Nchimbi alitoa rai hiyo jana katika kata ya Enaboishu iliyopo wilayani Arumeru mkoani hapa wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa sherehe za jando kwa vijana wa kiume wa rika la "Ilkishiru" zoezi lililoanza jana. Alisema kuwa hapa nchini makabila mengi yamepuuza mila na desturi zao ambapo alisema kwua Wamasai wanaongoza kwa kufuata na kutunza mila zao.

Aliyataka makabila mengine hapa nchini kuiga mfano huo wa wamasai kwa kuendeleza tamaduni zao kwa vizazi vyao na vijavyo. "Utamaduni huu wa kudumisha mila unatakiwa kuigwa na makabila mengine kwani tabia ya vijana kutojali na kutokuheshimu wazazi na wakubwa hao umekithitri hapa nchini hivyo kupitia mila na desturi hizo maadili yaliyoporomoka yatanogezeka"alisema Aidha aliwataka vijana kuhakikisha kuwa wanapodumsiah mila na desturi zao kuzingatia hali ya sasa ya dunia. Alisema kuwa hata katika zoezi hilo la jando,kuwashirikisha wataalamu wa kisasa wa tiba.

Nchimbi aliwataka kuhakikisha kuwa wanalinda rasilimali walizonazo ikiwa ni pamoja na kubadilika na kuweka mbinu za kisasa za kilimo na ufugaji bora ili waweze kuondokana na hali ya umasikini. Akisoma risala kwa niaba ya wenzake wanaokwenda jando Moikan Mesheti,alisema kuwa kuporomoka kwa maadili kunatokana na utandawazi uliopo hivi sasa huku vijana wengi wakikimbilia mijini kutafuta maisha
na kuacha shughuli za asili(ufugaji) maeneo ya vijijini.

Aliiomba serikali kuhakikisha kwua maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za mila na desturi kupewa hati miliki ili waweze kuhifadhi mila na desturi. Alisema kuwa kwa mila zao Rika hupishana kila baada ya miaka 14 ambapo zoezi hilo hufanyika,ambapo pia waliipongeza serikali kwa kudumisah mila na desturi.

Pia waziri huyo alijitolea kumsomesha kijana mmoja mwenye umri wa miaka saba aliyejulikana kwa jina la Edward Losanye mkazi wa Olkolada na nimwafunzi wa shule ya msingi Enguita anayesoma darasa la tano   ambaye  ndio kijana mdogo kuliko wate ambaye anapelekwa  jando .

"mimi najitolea kumsomesha huyu mtoto kuanza hapa alipo mpaka sekondari kwakuwa ndio kina mdogo anayejiamini na ameamua kwenda jando akiwa mdogo Tanzania tunaitaji vijana wakaka mavu na majasiri kama hawa amenifurahisha sana"Alisema 


Habari na Woinde Shizza,Arusha

Categories: