Baadhi ya wamachinga wakiwa wamelipindua gari yaina ya toyota na kusimama juu yake huku wakitamka maneno makali kwa polisi na jiji la mbeya kwa kuwanyanyasa katika biashara zao
Moja ya mabango waliyobeba wamachinga hao
Wamachinga wakiwazomea polisi eneo la kabwe
Maduka yote eneo la mwanjelwa mpaka uyole yamefungwa
Huu ndiyo mtaa wengi huuita mtaa wa kasisi uliyosababisha vurugu zote kati ya wamachinga na askari wa jiji
Mmachinga akiwarushia jiwe kwa kutumia manati yaani ni hatari tupu
Askari wa kutuliza fujo naye akiwarushia bomu la machozi wamachinga wanaoandamana
Naye mwandishi wetu wa mbeya yetu Joseph Mwaisango alionja joto ya jiwe baada ya kutupwa ndani ya gari ya polisi kwa kosa la kupiga picha matukio hayo ya wamachinga na polisi baadaye aliachiwa na kuendelea na kazi yake
Risasi za moto nazo zilitumika
mabomu ya machozi yalitumika zaidi
Hayo ndiyo maandishi yaliyoandikwa barabarani
kwa ufupi vurugu zinaendelea zimefika uyole kati hali si shwali barabara zimefungwa sasa nizaidi ya masaa 10 hakuna usafiri yati mbeya iringa wala mbeya tunduma habari kamili tutawaketea baadaye
Picha na habari na Mbeyayetu blog
Categories:
machafuko mbeya