Showing posts with label Pinda. Show all posts
Showing posts with label Pinda. Show all posts

PINDA NA WATALII MBUGANI KATAVI


 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Watalii kutoka Switzerland, Rolv (katikati ) na Erica kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi wakati alipokagua athari za kiangazi kwenye hifadhi hiyo. Picha na mdau Hilary Bujiku wa PMO
 

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

WAZIRI MKUU PINDA NDANI YA HIFADHI YA KATAVI

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama tembo wakati aliposimama kwa muda kwenye Lodge ya Katuma Bush katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi wilayani Mpanda wakati alipoitembelea kukagua athari za kiangazi kwenye Hifadhi hiyo Oktoba 20,2011.
Waziri Mkuu, Mizengo PInda akizama viboko waliosongamana kwenye tope baada ya mabwa na mito kukauka kuftokana na Kiangazi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi wilayani Mpanda Oktoba 20,2011.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Rais Jakaya Kikwete Amaliza Ziara Yake Mpanda na Kurejea Dar es Salaam

Rais Jakaya Kikwete akiwatazama wasanii wa kikundi cha ngoma cha Mtapenda cha Majimoto wilayani Mpanda(hawapo pichani) kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda kabla ya kuondoka kurejea Dar es salaam October 18, 2011. Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda .Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Rais Kikwete afungua Kongamano la Uwekezaji katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika Mpanda


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri mkuu Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawekezaji na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi hapa nchini muda mfupi baada ya Rais Kikwete kufungua kongamano la uwekezaji katika ukanda wa ziwa Tanganyika huko Mpanda mkoani Rukwa lao mchana.
(picha na Freddy Maro).
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akagua Madini Yanayochimbwa Mpanda



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua madini yanayochimbwa Mpanda wakati alipotembelea banda la TPM MINING COMPANY LIMITED katika maonyesho yatakayoambatana na uzinduzi wa mkutano wa uwekezaji unaotarajiwa kufunhuliwa na Rais Jakaya Kikwete Mjini Mpanda October 17,2011.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Taswira Za Muendelezo wa Ziara Ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda Nchini Marekani


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Rais wa zamani wa Brazil,Luiz Lula baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Marriott katika mji wa Des Moines, Iowa,Marekani October 13, 2011. Baadae Rais huyo alitunukiwa nishani ya Food Prize.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais wa World Food Prize, Balozi Kenneth Quinn wakifurahia baada ya Waziri Mkuu kutoa salamu za Rais Jakaya Kikwete kwenye Mkutano wa World Food Prize kwenye hoteli Marriott aktika mji wa Des Moines, Iowa, Marekani October 13,2011.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Pinda akunwa na teknolojia kilimo cha muhogo Brazil

Imeandikwa na Joseph Kulangwa, Sao Paulo


WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amekunwa na teknolojia ya kilimo cha muhogo, ambapo mashine maalumu zinatumika kupandia zao hilo tofauti na Tanzania ambako kilimo hicho bado ni cha kiwango cha chini na duni.

Waziri Mkuu alioneshwa kukunwa na teknolojia hiyo juzi alipotembelea kampuni ya kutengeneza vifaa na mashine za kilimo ya ABIMAC mjini hapa akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini Brazil.

Hata hivyo, alisema maendeleo hayawezi kupatikana bila kufanya kazi kwa bidii, lakini pia kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Alilazimika kusema hayo alipopewa fursa ya kufanya hivyo baada ya kuangalia video ya mambo yanayofanywa na kampuni hiyo yenye matawi katika mikoa 10 nchini hapa na kampuni tanzu 4,500.

Waziri Mkuu alisema kwa Tanzania teknolojia hiyo inapaswa kutekelezwa hatua kwa hatua na si kuikimbilia.

Akizungumzia juu ya teknolojia ya kilimo cha muhogo, Pinda alisema: “Tunaweza kutumia fursa hii kuboresha kilimo cha muhogo ... tunaweza kuula, lakini ni vema sasa nasi tukaanza kuuza nje pia,” alishauri.

Kuhusu mifugo, alisema teknolojia ya kutengeneza chakula cha mifugo kutokana na majani ya kawaida, miwa na mahindi, inaweza kuwasaidia wafugaji nchini Tanzania.

“Sisi kwetu Tanzania tuna mifugo takribani milioni 21, lakini Afrika kwa jumla tuna tatizo ... hali ya hewa inapobadilika tu mifugo hukosa chakula na kufa, lakini kwa teknolojia hii tunaweza kuiokoa,” alisema.

Naye Waziri wa Ardhi na Maji Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna ambaye anafuatana na Waziri Mkuu, alieleza kuvutiwa na teknolojia hiyo ya kilimo cha muhogo na chakula cha mifugo, akisema inaweza kuwasaidia Watanzania kama wataamua kuitumia kikamilifu.

Alisema teknolojia hiyo inaweza kusaidia wakulima na wafugaji kuinua hali yao ya kipato na hata kuondokana na umasikini lakini ikitumiwa vizuri.

Mbunge wa Rufiji, Dk. Seif Rashid alisema teknolojia hiyo inawezekana ingawa ni mpya, lakini akasema Watanzania wanaweza kufundishwa wakaielewa na kuitumia kujiendeleza.

Baadaye ujumbe wa Pinda ulitembelea kiwanda cha kutengeneza nishati ya ethanol itokanayo na miwa inayozalishwa na Kampuni ya Construtora Queiroz Calvao S/A.

Akiwa hapo hapo wilayani Piracicaba, Waziri Mkuu na ujumbe wake walitembelea kampuni nyingine ya Dedini ambayo licha ya kutengeneza mitambo ya kuzalishia ethanol inayotengeneza pia bidhaa mbalimbali za kiteknolojia pamoja na chakula na vinywaji.

Chanzo: Habari leo
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»