Showing posts with label tanga. Show all posts
Showing posts with label tanga. Show all posts

KAMATI YA BUNGE YA FEDHA NA UCHUMI YAFANYA ZIARA MKOANI TANGA

Mwengekiti wa kamati ya bunge ya fedha na uchumi,Abdala Kigodo (katikati) akieleza jambo kwenye ofisi ya TRA Tanga walipofanya ziara mkoani hapo. kulia ni katibu wa kamati,Maiko Kadebe na kushoto ni Kamishina wa forodha,Walid Juma.
Kamati ya bunge ya fedha na uchumi ikichangishana fedha za kusaidia ujenzi wa ofisi ya wajasiliamali walemavu wa viungo wa Mwamboni mkoani Tanga.kutoka kulia ni mwenyekiti wa kamati hiyo,Abdala Kigoda wa pili mjumbe wa kamati hiyo Dr. William Mgimwa na watatu ni Richard Ndassa mjumbe wa kamati hiyo pia.
Mjumbe wa kamati ya bunge ya fedha na uchumi,mbunge wa jimbo la Magogoni Pemba,Kombo Khamis Kombo akiongesha kiatu kilichotengenezwa na kikundi cha wajasiliamali walemavu cha Mwamboni mkoani Tanga.kushoto ni Mwengekiti wa kamati hiyo,Abdala Kigoda na kulia ni mwenyekiti wa walemavu,Ally Shekuwe walipofanya ziara mkoani hapo hivi karibuni.
Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiliamali cha Mwamboni mkoani Tanga,Ally Shekuwe kushoto akiteta jambo na mjasiliamali wa bidhaa za viatu Jackson Kingusa baada ya kupokea zaidi ya shs. laki tatu kutoka kwa kamati ya bunge ya fedha na uchumi za kukarabati ofisi hiyo ilipofanya ziara mkoani hapo
Benk ya NMB tawi la Madaraka mkoani Tanga limegawa fimbo 30 zenye thamani ya Shs. laki sita na arobaini kwachama cha walemavu wasioona mkoani Tanga
Kamati ya bunge ya fedha na uchumi ikitoka kuzuru jengo la bandari ya Tanga ikiwa ni sehemu ya ziara yao mkoani humo.
Jeshi la Polisi mkoani Tanga linavyo kabiliana na madereva wa pikipiki maalufu kama bodaboda kwa kubeba abiria wengi kinyume na utaratibu yaani mishikaki .
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Kilindi yakanusha kuingia ugonjwa wa kimeta

Imeandikwa na Anna Makange, Tanga

IDARA ya Mifugo na Uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, imewataka baadhi ya wafugaji na wananchi kwa ujumla kuacha kusambaza taarifa zisizo sahihi kwamba ugonjwa wa kimeta umeingia na kuua ng’ombe kadhaa.

Ofisa Mifugo na Uvuvi wa Wilaya ya Kilindi, Fredrick Kiango alisema hayo kutokana na kuongezeka kwa hofu miongoni mwa wakazi wa maeneo tofauti ya Mkoa wa Tanga zilizotokana
na tetesi kwamba ugonjwa wa kimeta umeingia wilayani Kilindi na kuua ng’ombe zaidi ya 100 hivi karibuni.

Kiango alisema ameshangazwa na taarifa hizo ambazo hata baada ya wataalamu katika idara yake kuzifanyia kazi vijijini, imebaini hazina ukweli wowote isipokuwa ni uvumi ambao hadi sasa hawafahamu lengo lake, na hasa kwa wananchi ambao ndio watumiaji wakubwa wa mazao yatokanayo na ng’ombe.

Alibainisha kwamba hivi karibuni katika baadhi ya vijiji vya wilaya hiyo ng’ombe 15 waliripotiwa kufa kutokana na ugonjwa wa chambavu na sio kimeta kama baadhi ya watu
wanavyosambaza uvumi na kudai kuwa tayari wametoa chanjo ya kudhibiti.

“Napenda ieleweke kwamba taarifa zinazoenezwa kuhusu kuingia kwa ugonjwa wa kimeta hapa Kilindi sio sahihi. Mwezi uliopita katika baadhi ya vijiji vyetu vinavyopakana na mikoa jirani,
ng’ombe 15 waliripotiwa kufa wakiwa na dalili kama za ugonjwa huo, lakini baada ya madaktari kukagua ile mizoga, walibaini ni ugonjwa wa chambavu ambao kimsingi baadhi
ya dalili zake zinafanana na za kimeta,” alisema.

Kiango alitaja vijiji hivyo kuwa ni Negero, Kimbe, Kilindi pamoja na Pagwi vilivyoko Tarafa ya Kimbe na kuongeza kuwa huenda baadhi ya watu hawakupata taarifa sahihi kuhusu matokeo ya kitaalamu ya uchunguzi wa vifo vya ng’ombe hao na hivyo kuamua kueneza hofu kwa
jamii na watumiaji wa mazao ya ng’ombe.

Aidha, alibainisha hatua zinazoendelea kuchukuliwa na idara yake hivi sasa ni kuendeleza utoaji wa elimu na chanjo kwa mifugo na kuwahimiza wafugaji kutoa taarifa mapema za
ng’ombe wagonjwa, kutogusa mizoga ya mifugo inayokufa kabla ya kumwita daktari ambaye akishabaini tatizo huwapa maelekezo sahihi.

Wakazi wengi wa Wilaya ya Kilindi wanajishughulisha na kilimo na ufugaji na kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana, wilaya ina mifugo ya aina mbalimbali zaidi ya 150,000, ng’ombe
wakiwa 145,000.

CHANZO: HABARI LEO
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»

Tanga yakumbwa na mafuriko

Imeandikwa na Anna Makange, Tanga

BAADHI ya wakazi wanaoishi kwenye maeneo ya mabondeni hususan katika mitaa ya Kata ya Mabawa katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, wamekumbwa na mafuriko kutokana na mvua iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo mwishoni mwa wiki.

Mvua hiyo iliyofululiza kwa zaidi ya saa 40 usiku na mchana, ilileta hofu si tu kwa wakazi hao wa maeneo ya mabondeni, bali hata katika maeneo ya katikati ya Jiji na kusababisha barabara kadhaa kutopitika kwa muda baada ya maji kujaa kutokana na mifereji kuzidiwa nguvu huku mingine ikiwa imezibwa na taka ngumu.

Wakazi wa kata hiyo, Mariam Adam na Sofia Waziri ambao wanaishi Magaoni, walisema mvua hiyo imesababisha usiku wakeshe kwa shaka ya kuingiliwa na maji nyumbani mwao.

Sofia alisema walilazimika kuvunja shughuli za uzalishaji badala yake walibaki nyumbani ili kujaribu kuchota maji hayo bila mafanikio huku wengine wakijitahidi kuweka vizuizi katika maeneo kadhaa ili kupunguza kasi ya mafuriko kuelekea kwenye makazi yao.

“Mafuriko hutokea kila mwaka zinaponyesha mvua maji mengi huingia kwenye mitaa yetu huku na hali hii tumebaini inasababishwa na uzembe wa baadhi ya watendaji katika Halmashauri hasa wanaohusika kushughulikia miundombinu ya mifereji midogo na mikubwa inayotiririsha maji taka na maji ya mvua kuelekea baharini kwa sababu imeziba kutokana na kujaa mchanga na taka ngumu,” alisema.

Kwa upande wake, mkazi mwingine, Saidi Ally alidai kuwa tatizo kubwa linatokana na viongozi kutowashirikisha wananchi wa maeneo hayo hasa vijana ambao hawana ajira rasmi kwenye kazi za kusafisha mifereji midogo inayoelekeza maji kwenye mifereji mikubwa kuelekea baharini, hatua inayowafanya wajione kwamba hawahusiki kwa kuwa wapo vibarua walioajiriwa kwa shughuli hiyo.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Mwembeni ‘B,’ Ernest Mussa alisema uzoefu unaonesha kuwa nyakati za kiangazi hakuna mtendaji anayejihusisha na usafi wa mifereji hadi maafa yanapotokea ndipo watendaji wa ngazi tofauti katika Halmashauri ya Jiji hujitokeza na vifaa hafifu ambavyo havina uwezo wa kukabiliana na mafuriko ambayo sasa yamekuwa kero kwao kila inaponyesha mvua.

Alisema ni vema mkakati endelevu wa kusafisha mifereji ya maji taka na ya mvua hasa ile mikubwa na midogo ikaendelea kuimarishwa wakati wote ili kusaidia kupunguza hofu ya madhara na kero zisizo za lazima zinazoendelea kusababisha mafuriko kwa wakazi wa Magaoni na Mwembeni.

Chanzo: Habaarai leo
[ Read More ]

Posted by newstz.blogspot.com 0 comments»