Na Gladness Mushi- Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye kwa sasa ndiye anayeshikilia wadhifa huo Bw Magesa Mulongo amesema kuwa kamwe hatakubali kuona mkoa wa arusha ukiwa unaangamia kwa ajili yabaadhi ya viongozi ambao si wazalendo wa nchi
Bw Magesa aliyasema hayo mapema leo wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mji wa arusha kwa mara ya kwanza mara baada ya kuchaguliwa kwake.
alisema kuwa ili kiongoiz kama kiongozi aweze kuitwa kiongozi ni lazima kwanza avae kofia ya uongozi na walasio kofia ya uchu wa madaraka kwa kuwa hali hiyo inafanya kazi nyingi kushindwa kufanyika kwa wakati huku wananchi wakiendelea kuumia.
Aliongeza kuwa hali hiyo kwa sasa ndani ya mji wa arusha itakwaisha kabisa kwa kuwa hata penda kwenda kufanya kazi aliyopewa na baadhi ya viongozi majina kwa kuwa mji wa arusha bado unakabiliwa na mambo mengi sana
Alisema kuwa kwa kiongozi ambaye hataweza kufanya kazi pamoja nay eye ni bora achie ngazi kwa kuwa viongozi wazembe ndio wanaochangia kwa kiwango kikubwa sana kuongezeka kwa changamoto nyingi ndani ya jamii ya watanzania
“leo mpo hapa wote napenda kuwaambia kuwa kamwe mimi sitaenda kwenye uongozi na mtu ambaye anajua anachokifanya kuwa ni kibaya na kwa hali hiyo leo nawatangazia wazi kuwa anayejijua kuwa anatabia ya kuwa moto baridi ni bora achie madaraka”alisema bw Magesa
Katika hatua nyingine aliwataka wakuu wa idara kuhakikisha kuwa wanafuatilia mambo mbalimbali ambayo yanafanyika kama vile miradi ndani ya miji na kata kwa kuwa baadhi ya wakuu wa idara ndio chanzo cha uharibifu wa kazi za jamii
Bw Magesa alisistiza kuwa hali ya kukaa tu ofisini kwa baadhi ya watendaji inafanya shuguli mbalimbali za kijamii kufanikishwa chini ubora wa viwango na watendaji wabovu kwa kuwa wanajua hawawezi kukaguliwa.
“leo unakuta mtendaji eti amekaa ofisini anapitisha malipo kwa mkandarasi sasa huyu mkandarasi jue kama amejenga chini ya ubora utajuaje lakini kama utakuwa unafuatlia na kukagua ujenzi na miradi mbalimbali hasara hazitatokea tena ndani ya miradi yetu”alieleza bw Magesa
Pia aliwataka madiwani wa jiji kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu wa kujua takwimu za miradi mbalimbali ambayo imo kwenye kata zao kwa kuwa nao baadhi ya madiwani hawana takwimu sahihi juu ya miradi
Mkuu huyo alisema kuwa madiwani wanatakiwa kujua na kutambua kuwa wanaiwakilisha serikali ikiwa ni pamoja na wananchi ambao waliwaamini na kuwapa kura kwa hali hiyo basiwanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafanya kazi sana bila kujali itikadi zao
Alimalizia kwa kusema kuwa endapo kama watafanya hivyo ni wazi kuwa jiji litakuwa na maendeleo mengi kwa kuwa mji wa arusha ndio kivutio pekee cha mji wa Tanzania.
Categories:
Mkuu wa Mkoa,
mkuu wa mkoa wa arusha